-->

Nay wa Mitego Akomaa na Young Killer Msodoki

Baada ya Young Killer kutoa ‘dis track’ aliyoipa jina ‘True Boya’ kumhusu Nay wa Mitego ambaye alimchana kupitia ngoma yake mpya ‘Moto’ Nay ameijibu kwa kukazia alichokiimba kwenye ngoma yake ni ukweli uliopo mtaani kwa mashabiki na wadau wa muziki.

Nay amefunguka na kusema kwamba hata diss track aliyoitoa Young Killer ni jingle kwani wimbo haujakamilika ingawa kwa upande wake alikuwa serious wakati anamchana kwa kuwa ni kweli hana makali kama aliyokuwa nayo awali wakati anatoka.

“Wimbo alioutoa Young Killer nimeusikia vizuri lakini kwangu ni jingle kwa sababu haujakamilika. Mimi nipo Serious na nilichokiongea kwa sababu watu wanaongea kwamba ana’drop’. Sasa kama kuongea ukweli ni kuchamba basi tutakuwa wengi sipo mwenyewe. Ni kweli kuandika anaandika vizuri lakini ni kama karudi hatua nyingi nyuma. Ninachozungumza  mimi hata yeye anakijua na hata wadau wa muziki wanaelewa” Nay alifunguka.

Aidha Nay ameongeza kwamba “Wasanii kama Baraka na Young Killer warudi nyuma wajue ni wapi walikosea na waombe radhi kwa watu waliowatambulisha kwenye game  kama hawapo nao sawa. Kama mtu alitoa muda wake hata kwa dakika kwa ajili ya kufanya jambo kwa ajili yako alafu baadae ukawa hauko nae sawa unatakiwa urudi nyuma na kujua wapi umekosea kwani hujui mtu alipoteza muda kiasi gani. Siku zote Discipline ndio kila kitu hivyo wajifunze” aliongeza Nay.

Pamoja na hayo Nay ameongeza kwamba upepo wa ngoma ya ‘Muziki’ aliyoifanya rapa Darassa haikumpatia Stress kwa sababu hata yeye aliwahi kuwa na hit song nyingi na bado ataendelea kuzitoa kila siku.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364