-->

Tuwe Wasafi wa Roho na Mwili – Lulu

Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ameoneshwa kukasirishwa na vitendo vya uchafu kwa baadhi ya waumini makanisani.

Lulu amesema waumini wawapo makanisani na hata nje wanatakiwa kuzingatia usafi wa mwili na roho kwani kuna muda huwa wanasalimiana wanapokuwa kwenye ibada hivyo kama hawatazingatia usafi huenda ikaleta taabu katika kukamilisha misa au ibada.

Mnaowekaga Vidole Puani Kanisani,Hamjui kama kuna ule muda wa kupeana mikono au Mnatakaga kugundua nini? Tuwe Wasafi Wa Roho Na Mwili Pia,“ameandika Lulu kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Hata hivyo mrembo huyo ameongeza kuwa kuna siku moja alimuona muumini mmoja akishika pua na leo ameamua kumpa makavu kwa kumuelimisha.

Wallahy kuna Mmoja alifanya hvyo Pembeni yangu leo Sijampa mkono bali Nimempa UKWELI,“ameandika Lulu.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364