-->

Nay wa Mitego Apewa Makavu na Mzazi Mwenzake

Msanii wa hip hop, Nay wa mitego amechezea kichambo kutoka kwa mzazi mwenzake ambaye ni muigizaji wa filamu za bongo, Skyner Ally kuwa ameshindwa kuwa baba bora kwa binti yake.

Kwenye ukurasa wake wa instagram Skyner amefunguka maneno hayo akiwa anamtakia heri ya kuzaliwa mtoto wake ambaye amefikisha miaka mitano na kudai kuwa alikuwa na dukuduku kutoka moyoni ndani ya miaka mitano na baada ya kuongea tayari limetoka.

“Thats face you make when you see your ‘daddy jina’ anakufanyia promotions na kudanganya watanzania kama Oooh my Twin sijui nanunua pisto, hata chupi unayovaa hajui thamani yake maskini. nimevumilia sana It’s 5 Years now nimejiskia kutapika na nimetapikaa.  Am done Mungu wa mbinguni nakuomba unijaalie maisha marefu uwezo nizidishie riziki….. uzima wa afya nikuleee mwanangu aje akuone baadae Inshallah umekuja kuwa Waziri wa nchi & Raisi wa nchi then alete pua yake” aliandika Skyner.

“Aidha skyner ameendelea kufunguka kuwa “Endelea na drama zako ila please shobo na mwanangu sitaki…Please unapost picha za mtoto wangu za nini…shobo dundo zanini? Sitaki shobo na mwanangu koma kama ulivyo komaaa…Je, Wababa anaojisifu kama wanapenda watoto wao then hata hawajui mtoto anakula nini anasoma wapi anavaaa nini Wapooooooo? Drama nyingi sana mtandaoni halafu i love You Nyingi Hana Analofanya Wapooooooooo ??? Am done”- Aliongeza Skyner.

Skyner hakuishia hapo  aliendelea kutoa husia kwa binti yake kwa kuonyesha jinsi alivyo na umuhimu katika maisha ya binti yake “Hakuna anayejua thamani yako zaidi yangu hata huyo anayejita baba’ko hana analolijua kuhusu wewe, si shule, malazi wala chakula kutwa kucha kukupost na kuongopea jamii kama anakujali, ninayehangaika nimie nakuhakikishia na kumuomba Mola wangu anijaalie uhai nguvu uwezo riziki nizidi kukulea kwa nguvu zangu Inshallah nakuonea gere sana umepata mama bora na sio bora mama uko mikono salama mwanangu wa uchungu. Happy Birthday My Happiness”- Skyner alimaza

Maneno hayo makali kwa Skyner yalikuja muda mfupi baada ya Nay kuweka picha ya binti yake na kumtakia heri ya kuzaliwa na kudai kuwa amenunua bastola kwa ajili ya kumlinda.

Hii ndiyo ‘Post’ ya Nay iliyosababisha mama watoto wake kumtolea povu kwa hasira.

eatv.tv

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364