-->

Nay wa Mitego: Naangaikia Kuupeleka Mziki Mbele Siwezi Kujibishana na Mtu

Rapa Nay wa Mitego anayetamba na kibao chake kipya kilichopewa jina la ‘Mikono Juu’ amefunguka na kudai hawezi kujibishana na mtu yeyote kwa sasa kwani yeye anachokihangaikia ni kupeleka mbele muziki wake ili watu wake waweze kuupata.

Nay ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo ‘PB’ inayorushwa na East Africa Radio na kusema kwa sasa amejikita katika kufanya kazi zake zaidi na sio kutafuta kiki kama wanavyofanya wasanii wengine.

“Sasa hivi sitaki kujibizana na mtu kabisa kabisa, ‘this time’ mimi nataka kufanya kazi zaidi ili nipeleke muziki wangu kwa watu wangu. Miaka miwili mitatu nyuma nilikuwa nafanya zaidi kazi hivi vitu vingine vilikuwa vinakuja nyuma. ‘This time’ nikiona mtu anaiingia kwa ajili ya kutaka kuleta kelele na mimi nampisha maana huo sio muda wangu”, amesema Nay.

Kwa upande mwingine, Nay wa Mitego amesema wimbo wake mpya kuchezwa kwenye bodaboda na sehemu mbalimbali ndicho alichokuwa anakitafuta kitokea na kudai hata vitu vingine vikija sio mbaya ili mradi muziki wake utangulie mbele.

VIDEOMPYA : TIWA SAVAGE- GET IT NOW

Bfya “PLAY” kuitazama

Comments

comments

Post Tagged with , ,

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364