-->

Ndoa 14 za Mastaa Bongo Mwaka Huu

2016 mwaka wa ndoa. Ndivyo ninavyoweza kusema kutokana kuwa mwaka huu wa baraka tele miongoni mwa wasanii wengi nchini kufunga ndoa tufauti na miaka mingine iliyopita.

Naweza kusema kuwa wasanii wengi walikuwa wanawoga wa kuingina kwenye ndoa na hata wengi kutunga nyingi kwamba suala hilo bado kama ‘Bado nipo kwanza’ wa Mwana Fa na ‘Nakula Ujala’ ya Ney Wa Mitego lakini mwaka huu wamefanya kweli.

Kwa sababu ndio tunaelekea mwishoni mwaka Swaggaz imeona si vibaya ikakuletea ndoa za wasanii zilizofungwa mwaka huu

January 9, 2016

Wastara na Sadifa

Aliyefungua uwanja kwa mwaka huu alikuwa ni Diva anayefanya vyema katika tasnia ya filamu za kibongo, Wastara Juma baada ya kufunga ndoa na Mbunge wa Jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma, licha ya ndoa hiyo kutodumu kwa muda mrefu.

Awali kabla ya ndoa hivyo Wastara alikuwa amefunga ndoa na marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia Januari 2013

April 9, 2016

Roma Mkatoliki na ‘Mama Ivan’

Baada ya kuishi na mchumba wake muda mrefu, Mamam Ivan, Mkali wa Hip Hop, Roma Mkatoliki aliamua kufunga pingu za maisha na mama mtoto wake huyo.

Ndoa hiyo ilihudhuriwa na mastaa wengi akiwamo Kala Jeremiah aliyekuwa best man. Wawili wakiwa tayari wana mtoto wa kiume, Ivan.

April 14, 2016

Mr blue

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Kheri Sameer maarufu Mr Blue, naye alifunga ndoa na mama wa watoto wake Waheeda.

Mr Blue na Waheeda walifunga ndoa kim ya kimya bila watu wengi kufahamu na inatajwa asilimia kubwa ya watu waliohudhulia ni ndugu wa familia ambapo walikuwa tayari wameshapata watoto wawili wa kwanza akiwa wa kiume na wa pili akiwa wa kike.

Mchekeshaji Mkono Mkonole

May 16, 2016

Kwa wale wanaofuatilia filamu jina la jian la msanii wa vichekesho, Mkono Mkonole si geni naye siku hiyo alianza kuitwa mume wa mtu baada ya kufunga ndoa kimya kimya mkoani Tanga na mwanadada, Sabrina Ally.

Mwana FA

June 5, 2016

Nyota wa muziki wa Hip hop, Khamis Mwijuma ‘Mwana FA‘ aliamua kujibu swali ala Mwana FA unaona lini? Kwa kufunga ndoa na mchumba wake Helga.

Ndoa hiyo ya ilihudhuriwa na ndugu na marafiki zake wa karibu wakiwamo AY, Hermy B, Ommy Dimpoz, Sallam, Dully Sykes, Alberto Msando na wengine.

June 6, 2016

Meninah na mwanaume mwingine

Mrembo aliyefanya vizuri na wimbo wa ‘Kakopi Kapesti’ na ‘Shaghala Baghala’, Meninah Atick, alifunga ndoa mara ya pili baada ya ile aliyofunga aliyofunga 2015 na Peter Haule, mtoto wa Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo.

Peter alibadilisha dini na kuwa muislamu ili kumuoa Meninah na kuanza kutumia jina la  Abdulkareem. Meninah alikuwa anatumia jina la Meninah Abdulkareem.

June 17, 2016

Riyama Ally na Mysterio

Juni 17 Riyama Ally aliingia kwenye listi ya wasanii wachache wa tasnia ya filamu waliofunga ndoa baada ya kufunga ndoa na aliyekuwa mpenzi wake wa siku nyingi Leo Mysterio ambaye ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva.

August 15, 2016

Masanja Mkandamizaji

Moja kati ya ndoa za mastaa zilizozungumziwa sana katika vyombo mbalimbali vya habari hususan mitandao ya kijamii ni ile ya Mchekeshaji wa Kundi la Orijino Komedi, Masanja Mkandamizaji na mwanadada Monica.

September 2, 2016

Shamsa Ford na Chid Mapenzi

Muda mfupi baada ya kuachana na msanii wa Bongo Fleva, Emanuel Elibarik ‘Ney Wa Mitego’, bidada anayefanya vyema katika upande wa filamu, Shamsa Ford ‘Shamsa’ alifunga ndoa na Mfanyabiashara maarufu wa mavazi, Chidi Mapenzi.

October 15, 2016

Tunda Man na Sabrah

Mkali wa wimbo ‘Mama Kijacho’ kutoka Tip Top Connection, Tunda Man aliuaga ukapela hivyom kuamua kufunga ndoa na mpenzi wake Sabrah.

Ndoa hiyo ambayo ilifanyika mkoani Morogoro nyumbani kwa Bi Sabrah, ikihudhuriwa na mastaa wa muziki kutoka Tip Top Connection.

 

October 29, 2016

Nyandu Tozzy

Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Kundi la BOB, Nyandu Tozzy naye mwaka huu amefunga ndoa kimya kimya na mpenzi wake wa muda mrefu.

Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Kiboko ya mabishoo’ alikuwa msanii wa pili ndani ya mwezi huu kufunga ndoa baada ya Tunda Man kuvuta jiko huko mkoani Morogoro.

Mabeste na Lisa Fickenscher

October 31, 2016

Msanii wa muziki wa hip hop Mabeste alifunga ndoa na mpenzi wake wa, Lisa Fickenscher na tayari wana mtoto mmoja Kendrick.

November 11, 2016

Nuh Mziwanda na Nawal

Mwaka huu haukumwacha nyuma mkali wa wimbo wa Jike Shupa, Nuh Mziwanda ambaye alifunga ndoa na mpenzi wake Nawal.

Nuh zamani alikuwa natoka na Mkali wa ‘Say my name’ Shilole Mohamed maarufu kwa jina la Shishi baby ambao waliachana mapema mwaka huu.

December 3, 2016

Chiwaman

Naye Mzazi mwenza wa msanii wa filamu Rose Ndauka, Maliki Bandawe aka Chiwaman alifunga ndoa kimya kimya na mrembo ambae jina lake halikupatikana.

Chiwaman ambaye pia ni msanii wa kundi la TNG na baba wa mtoto mmoja alizaa na Rose Ndauka waliachana na mwezi mmoja kabla ya tarehe yao ya kufunga ndoa.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364