Duma Awapongeza Gabo na Chuchu Hansy kwa Kunyakua Tuzo za EATV
Muigizaji wa filamu wa kiume Daudi Michael au Duma amempongeza muigizaji mwenzake Gabo Zigamba ambaye alikuwa naye kwenye kinyang’anyiro kimoja, na kuibuka na ushindi wa muigizaji bora wa kiume EATV AWARDS, huku akijipanga kupambana zaidi.
Kwenye ukurasa wake wa Instagram Duma ameyaandika haya kuhusu ushindi wa Gabo Zigamba.
Pia Duma alitumia fursa hiyo kumpongeza muigizaji mwenzake Chuchu Hansy ambaye amejishindia tuzo ya muigizaji bora wa kike EATV AWARDS.