Ndoa ya Lulu, Dj Majizo Yanukia
BAADA ya kuwa kimya kwa muda mrefu, staa wa filamu mwenye vituko vingi, Elizabeth Michael ‘Lulu’, ameibuka na kuweka wazi kwamba yupo mbioni kukamilisha maandalizi ya ndoa yake na mmiliki wa Redio EFM, Francis Shiza ‘Dj Majizo’.
Lulu, ambaye hivi karibuni alidaiwa kuachana na mpenzi wake huyo wa muda mrefu, aliliambia MTANZANIA kwamba taarifa hizo hazikumuumiza, ndiyo maana aliamua kuwa kimya, huku akiendelea na mipango yake ya ndoa na mpenzi wake huyo.
“Siku zinakaribia na karibu tarehe ya ndoa yangu itatangazwa kwa uwezo wa Mungu, hapo ndipo waliotamani tuachane wataziba midomo, maana natarajiwa kuwa mke halali hivi karibuni,’’ aliongea kwa madoido Lulu.
Lulu aliongeza kwamba, atakapoolewa amepanga kuwa mke mwema kama anavyoishi sasa kwenye hatua za uchumba.
Chanzo: mtanzania.co.tz