-->

Niachieni Mume Wangu, Sie Twazidi Kupendana!

Staa kutoka tasnia ya filamu Bongo, Riyama Ally, amewatolea povu wanaomfuatilia na kupenda kuchokonoa ndoa yake, kuhusu tofauti ya umri baina yak na mumewe, kwa kusema yeye na mume wake hawaachani ng’oo.

Riyama Ally akiwa na mumewe Haji Mwalimu Mzee ‘Leo Mysterio’.

Riyama amesema amechoshwa na baadhi ya watu wanaomsakama kila siku kuwa ameolewa na mwanamume mwenye umri mdogo .

“Huu ni uamuzi wangu kuolewa na mume ninayempenda, sijali umri wala mali zake ninachoangalia nini moyo wangu unapenda. Tuacheni jamani, sisi tunazidi kupendana,” alisema Riyama.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364