-->

Nido za Kajala Zageuka Gumzo!

Staa ‘the big name’ wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ amegeuka gumzo ukumbini kufuatia kupita mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwa amebusti nido (matiti) kiasi cha kuwafanya baadhi ya waalikwa ‘kumdiskasi’.

KAJALA78

Tukio hilo la aina yake lilijiri usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita ndani ya ukumbi wa sinema uliyopo Jengo la Quality Centre Barabara ya Pugu jijini Dar ambapo staa huyo alikuwa akizindua filamu yake ya Sikitu huku mgeni rasmi akiwa Waziri Nape.

Katika shughuli hiyo ambayo Wikienda lilikuwa ndani ya nyumba, baadhi ya wapenyeza ubuyu walisikika wakinong’onezana juu ya matiti ya Kajala namna yalivyokuwa yametuna kwenye gauni tofauti na alivyozoeleka kiasi cha wengine kudai ameyabusti kwa kuyachoma sindano.

“Mh! Jamani mbona leo Kajala amebusti nido kiasi hiki? Si bure, kama hajachoma sindano ya kubusti itakuwa si bure. Yaani unaambiwa watu wanamkodolea mimacho hadi wanaduwaa,” alisikika mmoja wa mashabiki aliowaalika kwenye sinema hiyo ambayo itakuwa gumzo mtaani.

kajala-992

Shuhuda mwingine alisikika akisema kuwa, Kajala aliwafanya hata wasanii wenzake kumgeukia wakati anaingia ukumbini hasa wengi wao walikuwa wamemkodolea jicho kifuani kwake kwa lengo la kutaka kuona namna alivyokuwa amebusti nido.

Alipofuatwa Kajala kuulizwa kulikoni au nini kimetokea hadi akavimbisha matiti kiasi hicho, hakuwa na la kusema zaidi ya kushukuru kwa kufana kwa uzinduzi wa filamu yake hiyo.

“Hivi huna ‘engo’ nyingine? Huoni watu wanavyoifurahia filamu yangu? Hayo ndiyo mambo ya kuniuliza,” alisema Kajala akisisitiza kuwa hataki maswali zaidi.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364