-->

Nikki wa Pili awapa makavu wasanii

Msanii kutoka kampuni ya Weusi Nikki wa Pili amefunguka na kuwachana wasanii wenzake ambao wanapuuzia vikao vinavyoitishwa na kudai endapo hawatobadilika na tabia hiyo basi watambue haki zao zitachelewa kuwafikia.

Nikki amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya yeye kuchaguliwa kuwa miongoni mwa wasanii wa kusimamia mfuko wa wasanii wa bongo fleva ambao utawasaidia wasanii watakao kuwa wanahitaji fedha kutoka katika mfuko huo.
“Wasanii ambao wanapuuzia kuja katika vikao nawaambia haki zao zitachelewa kuja, mpaka pale mtakapoamua kukaa mstari wa mbele haki ndipo zitakuja lakini mkiendelea kukaa hivyo mtatoa nafasi kwa watu wengine kutengeneza sheria ambazo zitakuja kuwaathiri”, alisema Nikki wa Pili.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364