-->

Nilifanya muziki nipate mademu – Dully Skyes

Msanii Dully Skyes ambaye sasa anafanya vyema na ngoma yake ‘Yono’ amefunguka na kusema kuwa yeye alianza kufanya muziki wa bongo fleva ili awe mtu maarufu na kuanza kupata wanawake.

Dully Skyes alisema hayo leo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio kwenye Heshima ya bongo fleva na kusema miaka kumi na kitu iliyopita aliamua kuingia kwenye muziki na kuwa msanii ili apate wanawake.

“Mimi niliamua kuwa msanii ili kwanza niwe maarufu nipate mademu tu na kupendwa na wasichana kwa hiyo wala sikufikiri kuwa msanii ili nipate pesa ndiyo maana hata nilipolipwa elfu mbili kwa ajili ya show nilikubali japo nilitakiwa kulipwa elfu tano, tena hiyo elfu mbili niliona nyingi na nikamlipa Queen Darleen mia tano sababu nilikwenda naye kwenye show. Kwa hiyo sikuwahi kufikiria kama muziki ungekuwa biashara kama ilivyo sasa, saizi nafanya muziki biashara ikitokea hao wanawake wametokea ni ‘by the way’ tu” alisisitiza Dully Skyes

Dully Skyes ni moja kati ya wasanii ambao atakuwepo kwenye tamasha la ‘Heshima ya bongo’ fleva ambalo litafanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 1/7/2017 katika ukumbi wa Dar Live Mbagala ambapo wasanii wengine kama TID, Dudubaya, Juma Nature, Z Anto, Solid Ground Family, Mabaga Fresh, Mandojo na Domokaya na wasanii wengine watawasha moto kwa ngoma zao kali za zamani.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364