-->

Nilijua Leo Tungeambiwa Roma Amepatikana – Mpoto

Msanii Mrisho Mpoto leo asubuhi na mapema alikwenda Kituo Kikuu cha Polisi (Central) ili kufuatilia sakata la kutekwa kwa msanii Roma Mkatoliki, Moni Centrozone na wenzao wengine wawili akiwepo producer Binladen pamoja na Emma.

Mrisho Mpoto anasema alikwenda leo asubuhi na mapema akiwa na matarajio kuwa huenda polisi leo wangeweza kuwapa taarifa kuwa wasanii hao wamepatikana lakini kwa mujibu wa taarifa ya Kamishna Simon Sirro ni kwamba mpaka sasa wasanii hao hawajapatikana na hawafahamiki wapo wapi, ila amesema bado wanaendelea na upelelezi.

“Sisi kama wasanii tunaendelea kusikitishwa na kuumizwa na suala zima la Roma Mkatoliki na ndiyo maana nimekuja hapa asubuhi na mapema nilikuwa najua kwamba tutaambiwa Roma amepatikana yupo hapa salama na vitu kama hivyo, kwa hiyo matarajio na nilichokisikia vimetofautiana lakini siwezi kuingilia mamlaka,” alisema Mrisho Mpoto 

Mbali na hilo Mrisho Mpoto ametoa wito kwa jamii

“Wito wangu kwa jamii ni utulivu na kuendelea kumuomba Mungu na kuacha waandishi wa habari na vyombo husika viweze kufanya kazi zake” alisema Mrisho Mpoto 

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364