-->

Nuh Mziwanda Afungukia Kilichomkutanisha na Shilole Huko Zenji

Msanii wa bongo fleva Nuh Mziwanda amesema Shilole ni msanii mwenzake na walivyoenda Zanzibar hawakuwa pamoja kila mtu alikuwa ameenda kwa kazi yake.

Nuh na Shilole katika moja ya matukio ambayo wamewahi kukutana baada ya kuachana

Akipiga story kupitia eNewz ya EATV Nuh Mziwanda amesema hata kama akiamua kutoka nje ya ndoa siyo lazima atoke na Shilole kwakuwa wanawake ni wengi na anapokuwa  kwenye show huwa anakutana na wanawake wengi hivyo siyo lazima atembee na Shilole..

Hata hivyo Nuh Mziwanda amesema haoni sababu ya kutoka nje ya ndoa yake na mashabiki zake wanapaswa kuelewa kwamba anapokuwa kwenye show moja na Shilole ni kutokana na maslahi hawezi kukataa pesa eti kwa sababu show aliyopata Shilole yupo.

Pia Nuh alimalizia kwa kusema “Zanzibar kila mtu alienda kwa kazi zake japo tulijikuta tumeshukia hotel moja, Shilole akiwa ameenda kuzindua Pub lakini mimi nilikuwa nimeitwa na nimepewa pesa zangu kwa ajili ya kufanya show”

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364