Nimekosea Wapi? Kuonyeshwa Suncrest Quality Centre Kwenye Big Screen!
FILAMU kubwa ya kitanzania ya Nimekosea wapi? ya mtayarishaji na mwigizaji mahiri Swahilihood Salum Saleh ‘Fizo’ itakuwa ni filamu ya kwanza kufungua njia kuonyeshwa katika jumba la sinema la Suncrest Cineplex Cinema lilopo Quality Centre wiki ijayo.
Akiongea na FC Fizo amesema kwake ni bahati kubwa sana kupata nafasi hiyo kwa filamu yake kuwa ya kwanza kutoka kampuni ya Steps Entertainment kuanza kuonyeshwa katika Jumba la sinema katika Big Screen na kuingia katika hatua nyingine ya biashara.
“Namshukru sana Mwenyezimungu kwa kupata bahati hii nimetengeneza filamu kubwa na inaonyeshwa katika ukumbi wa filamu kwa hadhi kubwa, nipo na wasanii wakubwa Gabo zigamba na wengine,”anasema Man Fizo.
Filamu ya Nimekosea wapi? inatarajia kuonyeshwa tarehe 11.May.2016 kwenye Bongo Movie Premiere kuanzia saa 1:00 ambapo wasanii watapita katika Red Carpet na kuingia ukumbi kwa ajili ya kuona sinema yenye ubora mkubwa.
Tarehe 12.may.2016 hadi tarehe 15. May. 2016 saa 2:00 kamili usiku kila siku sinema ya Nimekosea Wapi? itaonyeshwa katika ukumbi wa Suncrest Cineplex Cinemas na wapenzi wa filamu kujionea hatua kubwa kutoka kwa wasanii wa kitanzania wakifanya mambo makubwa.
Na tarehe 16. May. 2016 filamu ya Nimekosea wapi itaingia mtaani kwa maana hatua ya Dvd.