-->

Niombeeni Dua-Mzee Yusuph

Alhaji Mzee Yusuph, amefunguka kwamba wananchi wamuombee dua ili aweze kupata moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki alichofiwa  mke wake  Chiku Khamisi pamoja na mtoto wake mchanga  badala ya kuanza kuongea maneno ya unafiki yasiyokuwa na faida.

Alhaji Mzee Yusuph

Alhaji amefunguka hayo mara baada ya kuwapumzisha vipenzi vyake hivyo makaburini na kusema kwamba badala ya watu kuanza kuzungumza maneno ya unafiki, watumie muda huo kutafakari matendo yao duniani, ikiwa ni pamoja na kuwaombea dua waliotangulia pamoja na yeye aendelee kuwa jasiri.

“Niombeeni dua niwe na moyo wa subira, huu ni mtihani mkubwa sana ulionitokea. Muombeeni mke wangu pia aliyetangualia. Namshukuru Mungu mtihani umekuja kipindi ambacho nmemrudi kwaake laiti kama ningekuwa badio na mambno ya dunia sijui hata leo kingezungumzwa kitu gani” , alisema Mzee Yusuph.

Aidha Mzee Yusuph amekiri kwamba ameshakumbana na mitihani mingi tangu abadilishe muenendo wa maisha yake lakini kuhusu suala la kuondokewa na mke pamoja na mtoto mchanga ni pigo kubwa ambalo mpaka sasa haamini.

Mitihani mingi niliyoipitia haijanishtua lakini huu wa sasa mpaka sasa siamini nahisi kama bado naota, niombeeni nipate ujasiri nifaulu maana nikifeli katika hili nitakuwa sina tena dini” , Mzee Yusuph alisisitiza.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364