-->

Sijafuata Utaratibu wa Alikiba – Abdu Kiba

Msanii wa Bongo Fleva, Abdu Kiba amesema hajafuata utaratibu wa kaka yake ‘Alikiba’ wa kutomfollow mtu yeyote katika mtandao wa instagram.

Muimbaji huo amesema kilichopelekea yeye kutomfollow mtu yeyote ni baada ya wadukuzi kuiba akauti yake na alipoirejesha ilimbidi kuwaondoa watu wote waliokuwepo.

“Nikizungumzia akauti nakumbuka mwezi mmoja nyuma nikiwa Marekani akaunti yangu walihack kwa hiyo nilikaa karibia wiki tatu siko kwenye mtandao wa instagram, nilipoweza kuirudisha akauti yangu ndipo nilipoamua nisimfollow mtu yeyote kwa sababu watu niliowakuta mule sio watu wangu,” amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“Kwa hiyo niliwa-unfollow nikabakia siwezi kumfollow mtu tena. Sijafuta utaratibu wake bali ni maamuzi yangu, wategemee any day naweza nikamfollow mtu yeyote,” amesema Abukiba.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364