-->

Nisha Kufutrisha Watoto Waishio Katika Mazingira Hatarishi!

Nisha akiwa na wanahabari akiongelea kufutrisha watoto yatima,watoto waisho katika mazingira hatarishi

Nisha akiwa na wanahabari akiongelea kufutrisha watoto yatima,watoto waisho katika mazingira hatarishi

Asallam aleykhum Wanahabari,
Kampuni ya Nisha’s Film Production inapenda kuujulisha Umma kuwa inatarajia kuwakutanisha Watoto Waishio katika Mazingira Hatarishi walio ndani ya jiji la Dar es Salaam, kwa ajili ya Futari tukio hili litakalofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Azani Siku ya Jumapili tarehe 26 June 2016 na kujumuika pamoja kwa kuwapa faraja na kusikia changamoto zinazowakabili watoto hawa ambao ni jamii yetu inayohitaji faraja kutoka kwetu.

Nisha’s Film Production iliyo chini ya Mkurugenzi Salma S. Jabu (Nisha) ni watengenezaji wa filamu pamoja na uandaji wa matamasha mbalimbali ya wasanii ambayo yanalenga kuelimisha na kuburudisha jamii, mimi ni balozi wa Watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi hapa nchini hivi sasa nimeteuliwa kuwa msimamizi mkuu wa kituo cha kulelea watoto wasio kuwa na hifadhi kutokana na changamoto mbali mbali za kijamii, kituo kinaitwa NEW HOPE FAMILY kilichopo Kibada Mwasonga hapa Dar es salaam.

“Wito wa Dini yetu hasa kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, waislamu tunapaswa kutoa Dhaka pamoja na kuonyesha upendo kwa wenzetu wanaoishi katika mazingira magumu hasa watoto Yatima, Walemavu, wanaoishi mitaani pamoja na watoto wenye Ulemavu wa ngozi kwa kushirikiana nao katika shughuli mbali mbali ambazo zinaweza kuwa ni sehemu ya faraja kwao”.

Mimi kama muumini wa kiislamu na niliyelelewa na kukulia katika Dini nimeona ni vyema nije hapa kuzungumza nanyi wanahabari kwa sababu ndio kiunganishi chetu kikuu katika masuala ya kijamii. Kwa dhamira moja ya kuujulisha umma wa Kitanzania kuwa kupitia kampuni yangu ya NISHA’S FILM PRODUCTION tunatarajia kuanda futari ya pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi hapa jijini Dar es salaam, tukiwalenga zaidi watoto wanaoishi katika vituo vya kulelewa pamoja na wale ambao wapo mitaani na hawana sehemu za kuishi.

Futari ambayo itafanyika siku ya jumapili June 26, 2016 katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Azania kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa 2:00 usiku ambapo tunatarajia kuwepo na viongozi wakuu wa Serikali kama vile Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Bi. Samia Hassan Suluhu, Mbunge wa jimbo la Ilala Mh. Mussa Hassani Zungu, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, viongozi wa Dini pamoja na wasanii na watu Mashuhuri hapa nchini ambao watashiriki kwa pamoja na watoto hao katika futari hiyo.

Hadi sasa tuna mshukuru Mwenyezi Mungu maandalizi yamekamilika kwa kiwango kikubwa kwani tumeandaa utaratibu wa kuwafikia wale ambao wanaishi maeneo ya pembezoni mwa Jiji letu tutawasafirisha baadhi ya watoto waliopo kwenye vituo vilivyopo huko tukitarajia kuwepo na ulinzi pamoja na usalama madhubuti.

Hivyo basi NISHA’S FILM PRODUCTION tuna chukua nafasi hii kuwakaribisha watu wote ambao wanaishi katika mazingira hayo pamoja na kuiomba jamii kutusaidia ili tuweze kuwafikia watoto ambao wapo mitaani pamoja na wale ambao wapo katika vituo vya mbalimbali ili nao wapate kushiriki, wanaweza kutupa taarifa kupitia namba……..

Napenda kuchukua fursa hii kuwashukru sana wanahabari nikiamini pia nanyi mtakuwa mabalozi wanzuri katika harakati hizi za kuhakikisha tunamaliza matatizo haya ambayo yanaizunguka jamii yetu hasa watoto hawa wasio na hatia yoyote lakini leo wamekuwa wahanga wa matatizo ya familia zetu, TUWAPENDE, TUWASIKILIZE, TUWASAIDIE, TUWAFARIJI naamini wana haki ya Kuishi, wana mahitaji muhimu kama watoto wengine, Pia wenzetu wenye matatizo ya Ngozi TUWALINDE TUWAPENDE.

FC

NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

KAMA WEWE NI MFANYA BIASHARA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364