Nisha: Majungu, Wivu Vilinitenga na Marafiki
Staa wa sinema za vichekesho Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amefunguka sababu za yeye kutokuwa na marafiki wa kike kuwa ni majungu na wivu tofauti na marafiki wa kiume.
Nisha ameliambia Wikienda kuwa, watu wengi wamekuwa wakimuuliza sababu ya kuwa na marafiki wa kiume pekee na siyo wa kike ambapo amekuwa akiwajibu kuwa si kwamba hakuwahi kuwa nao lakini aliachana nao kwa sababu wanawake wengi hawawapendi wenzao kwani wakiona wanafanikiwa huwa wanaumia.
“Niliyoyapitia kwa marafiki wa kike ni tofauti na wa kiume, wa kike wana wivu na majungu mengi, mtu ukimpita kidogo tu kimaendeleo anakuwa na chuki tofauti na wanaume,” alisema Nisha.
Nisha aliweka wazi kuwa marafiki wa kiume ni muongozo mzuri kwa sababu ukishuka wanakuongoza na ukiwa nacho bado mnasaidiana tofauti na baadhi ya wanawake.
Chanzo:GPL