-->

Niva Amepata Shavu la Kufanya Kazi na Msanii Mkubwa wa Marekani (Video)

Msanii wa filamu Niva Super Mariyoo, amefunguka kwa kudai kuwa amepata mwaliko na msanii mkubwa wa Marekani kwajili ya kushiriki kwenye filamu yake.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Niva amedai ofa hiyo imemfanya arudi darasani kwajili ya kujifunza kuongea kingereza.

“Mtegemee kumwona Niva kimataifa zaidi ndani ya mwaka huu kupitia kampuni mpya ya Barazani, tayari kuna wasanii wa Marekani ambao wamehitaji kufanya filamu na mimi tena sio wasanii wadogo,kwahiyo mashabiki wakae mkao wa kula kuna makubwa yanakuja,” alisema Niva.

Aliongeza, “Lakini ninachokifanya kwa sasa narudi darasani kusoma kingereza cha kuongea, kwa sababu naamini ili ufanye kazi nzuri na wale watu lazima uwaelewe vizuri wanachokizungumza,”

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364