Nora Afungukia Wasanii Kujiuza
MKONGWE katika fi lamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ ambaye kwa sasa anajishughulisha na ujasiriamali baada ya soko kwenda halijojo, amedai biashara ya kujiuza inayofanywa na baadhi ya mastaa wa tasnia hiyo hailipi na itawaathiri zaidi baadaye.
Akipiga stori na Za Motomoto News, Nora alisema ni vyema wakatafuta shughuli halali ya kufanya ili kujipa heshima na hadhi ya majina yao kuliko kuishi kwa kujiuza kwani wanadharaulika na kusemwa vibaya na wanaume wanaowachukua.
“Nafanya biashara ndogondogo za kuuza nguo za watoto na saluni hivyo nawasihi wasanii wenzangu wa kike waachane na biashara ya kuuza miili yao, kwani ni hatari na ina madhara makubwa,” alisema msanii huyo wa siku nyingi.
Chanzo:GPL