-->

Nuh Mziwanda Abadili Dini, Amkacha Mke

Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Nuh Mziwanda amethibitisha kurudi katika dini yake ya awali ya Ukristo na kutengana na mkewe.

Kupitia XXL ya Clouds FM, Nuh ameeleza kuwa ni kweli alikuwa kanisani siku ya Jumapili kama taarifa zilivyozagaa katika mitandao mbalimbali kuwa ameonekana kanisani.

“Nimerudi kwa Mungu wangu ili mambo yangu yaende vizuri maana tunafanya muziki wa dunia anatusamehe ila kurudi kwake pia ni jambo la kawaida sana,” amesema Nuh.

Pia msanii huyo amekanusha taarifa zilizotolewa na aliyekuwa mke wake kuwa ameacha kumjali mtoto wake Anyagile tangu watenganae na kusema tuhuma hizo hazina ukweli.

“Mara ya mwisho nilikuwa na Anyagile kwenye photoshoot ya ngoma yangu mpya jana kwa Mx Carter, inayotoka hivi karibuni sasa yeye anavyosema sijamuona mtoto muda mrefu sijui anamaanisha nini, ” amesema Nuh.

Pia ameongeza kuwa “Anaongea vibaya kwenye media sio vizuri, mimi na fan base yeye mwanamke anatakiwa ajue anaongea nini, ila muache aongee akikua ataacha, vile vile mimi sina tatizo naye kama kaolewa, yeye si ndio kaamau mimi bado kijana na kila mtu anafanya anachotaka mimi nimemrudia mungu huwezi jua atanipatia mke mwingine mwema”.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364