-->

Wolper Awapa Ngumu Kumeza Instagram

Kupitia ukurasa wake wa Instagram,muigizaji Jacqueline Wolper ameandika kupitia ukurasa wake Instagram.

Hivi ni nani asiekuwa na furaha instagram, kila mtu hujitia mapenzi mazuri, maisha mazuri, hakuna magomvi ndani ya nyumba wakati in reality watu wanalia kimyakimya tunawachora, wengine wanapigika wee bila kusahau mikopo kibao mpaka usiku wanaota wanakimbizana na marejesho lakini wakija insta wanajitia wao eti wako perfect huku wanakufa na tai shingoni tena kwa kupotray uongo, sio lazima maisha yako uyaweke insta lakini pia hakuna ulazima wa kudanganya ukweli wakati mambo yenu yako hadharani, mbona tunajuana mjini apa.

 

Sasa naomba niongee kwa sauti na nieleweke, nimeamua kuwa open book, haya ndio maisha niliyoyachagua mimi jacky, bila kusahau nimeamua kuishi maisha yangu na kujipa furaha bila kujali kingine chochote, sasa nyie mnaosema huyu hafai hebu nionesheni mabwana zenu wanaofaa, na mbona mnaocomment wengi wenzangu tu ila ndio mnalinda status, wengine mnajikongoja ndani hata cha maana hampewi mnafichia siri bwana kulinda heshima mtakufa, na bado wanaume zenu wanawacheat pia tunajua tena wanawacheat huku wanawaongelea vibaya, haya maisha tunafanana tu tofauti yangu nimeweka wazi, tena huenda yangu ni bora, haya nyie mnaosema huyu mdogo mkisikia natoka na baba zenu wazazi mtapenda kweli, nipeni mabwana zenu basi walio perfect tushee

 

Kiufupi wote mliofurahi post za usiku nilikuwa nataka kujua ushambenga wenu nauzushi wenu mtazusha nn nakweli mmeyazua nimezoom comment zeu nanimejua maombi yenu pia niwape tuu big’up kwamafunzo miliyosomea nakma mngekuwa mnajua kazi kma umbea naroho mbaya tungekuwa madon? nikiachwa pia mtajua maana mi sio wa kwanza wala wa mwisho duniani nasijuag kuficha? wengine hata mama zenu waliachwa ila mko insta kung’ang’ania ya watu

Usiforce tufanane haya ni maisha yangu ni nitayaendesha vile ninavyojisikia sisi bado tupo sana tu kwasasa jamani, huyu asiefaa ndio nampenda mimi ili kuepusha foleni maana anaefaa itakuwa stress jamani, hafai wa kwangu, mdogo wa kwangu, hana hadhi yangu wa kwangu mimi, mimi ndio ninajua ninachokitaka maana haya ni maisha yangu, hata wa mwanzo si mlisema hana hadhi mbona mnamuoana wa maana sasa!! Kila mtu ashike lake jamani kwa huyu Nimeshindikana
ACHENI MAIGIZO KWENYE COMMENT ZENU

Wolper Instagram.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364