Nuh Mziwanda: Bora Shilole Kuliko Petit Man
Msanii wa Bongo Fleva Nuh Mziwanda kwa sasa ameingia katika mgogoro na aliyekuwa meneja wake, Petii Man kutokana na madai kuwa Petii Man amekuwa akitumia jina lake vibaya kupiga hela.
Nuh alitumia dakika 4 akiiambia eNewz kuwa Petii Man alikuwa ni mpigaji, na hakuwa na mchango wowote katika kuuendeleza muziki wake, huku akimkumbuka mpenzi wake wa zamani kwa kusema “Mtu wa kumshukuru katika muziki wangu ni Shilole na si Petit Man”.
Nuh aliongeza “Nilishapoteza miaka mitatu kwa ishu za mapenzi sasa siwezi kupoteza mwezi mmoja kwa mtu ambaye hana mchango wowote kwangu na kanikuta tayari nimeshakuwa star, siwezi kufanya kazi na yeye kwa sababu hatuendani na anachukua hela kupitia mgongo wangu bila mimi kujua na pia ni meneja ambaye yeye anahangaika zaidi yeye mwenyewe kuwa star”.
Pia Nuh alitambulisha Studio yake mpya aliyoipa jina la L.B RECORDS huku akijibu watu wanaosema kuwa studio hiyo ndiyo imefanya angombane na meneja wake (Petii Man) kwa kusema “studio hii ni jasho langu na haihusiani na ugomvi wetu”.
eatv.tv