-->

Dude: Tasnia ya Filamu Bongo ni Kama Choo cha Jiji

Msanii wa filamu nchini, Kulwa Kikumba aka Dude, amesema tasnia ya filamu Tanzania imekuwa kama choo cha jiji ambapo kila mwenye hela na anayetaka kuwa maarufu, hukimbilia huko.

dude35

Kulwa Kikumba aka Dude

Dude amesema hiyo ni sababu kubwa ya kuzorota kwa tasnia ya filamu nchini.

“Ubovu wa kazi za movie unakuja kutokakana na kupenda hela zaidi kuliko kufikiri,” Dude aliiambia E-News ya EATV.

“Leo hii Diamond anafanikiwa kwasababu anafikiri zaidi, ndio maana anenda kimataifa lakini huku kwenye movie kumeingiliwa. Leo hii mtu mwenye hela yeyote akitaka kuwa maarufu tu anakimbilia huku na anakuwa producer kabisa. Yaani pameingiliwa kama choo cha city vile,” alisisitiza.

“Inabidi lazima tuanzishe vyombo strong ili ukitaka kuingia huku kwenye movie lazima pawe kama ukitaka kuingia chuo kikuu vile. Na wasanii siye ambao tumejulikana tuache kubweteka, tufanye kazi nzuri siyo tu ilimradi.”

Bongo5

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364