-->

Nyie Acheni Kumpakazia Diamond

KAMA kuna habari inayobamba kwa sasa katika mitaa ya Jiji la Dar es Salaam basi ni ishu nzima ya Diamond Platinumz.

Jamaa amekuwa gumzo kutokana na kuwepo kwa taarifa kwamba kidume kimefanya yake kwa kuwajaza mimba warembo Hamisa Mobetto na Peneal Mwingilwa aliowahi kutoka nao kimapenzi kabla ya kujituliza kwa Zari the Boss.

Warembo hao wamekuwa wakichukuliwa picha zao na mashabiki wao na kupostiwa katika mtandao wa Instagram huku wakizungushiwa duara katika tumbo na kuambiwa tayari Diamond kushafanya yake, wakimkebehi kiaina Zari.

Hata hivyo, ukweli ulivyo ni kwamba, hata kama Diamond alishapita anga hizo, kwa sasa vimwana hao wana maisha yao na wapenzi wao, hivyo waache wasiharibiwe mambo.

Tayari warembo hao wameshaziruka taarifa hizo za kubebeshwa vibendi na Chibu Dangote, huku wakisisitiza kuwa, kwa sasa wao na Diamond ni marafiki tu kimtindo.

Chanzo:Mwanaspoti

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364