Ochu Shegy ni Bora Kuliko Chris Brown – Witness
Rapa wa kike nchini, Witness a.k.a kibonge mwepesi amefunguka na kusema kuwa msanii Ochu Shegy ambaye kwa sasa ni mume wake kuwa yeye ni bora kuliko hata Chris Brown.
Witness alisema hayo kupitia kipindi cha 5Selekt kinachorushwa na Ting’a namba moja kwa vijana na kudai kuwa kwa sasa Ochu Shegy ni kama ‘Role Model’ wake ambaye amemjenga na kumfanya kuwa mtu wa aina nyingine.
“Kiukweli Ochu Shegy is the best kuliko hata huyo Chris Brown, kwangu mimi Ochu saizi amekuwa ‘Role model’ wangu maana amenijenga sana na kunifanya kuwa wa tofauti sana’ alisema Witness
eatv.tv