Picha: Barakah The Prince Aonyesha Mjengo Wake wa Kisasa
Msanii wa bongo fleva nchini Tanzania ambaye aliwahi kupata tuzo ya msanii bora anayechipukia mwaka 2014 /2015 kupitia wimbo wake ya ‘Jichunge’ Barakah The Prince ameonesha matunda aliyoyapata kutokana na muziki tangu aanze kuimba mwaka 2014.
Miongoni mwa mafanikio aliyopata ni pamoja na kujenga nyumba kubwa yenye vyumba 5 huku nje akiwa ameweka sehemu ya kuogelea (Swimming Pool)
eNewz ilipiga naye story katika site yake hiyo aliyoijenga maeneo ya Tegeta jijini Dar es Salaam akiwa na mpenzi wake wa sasa, Naj ambaye pia ni msanii wa bongo flevana kusema kuwa wametumia fedha nyingi sana kwenye hiyo nyumba na bado haijakamilika na kwamba hayo ni matunda ambayo ameyapata kutokana na kazi ya muziki na ushirikiano na mpenzi wake huyo.
“Namshukuru sana mke wangu Naj kwa sababu ana mchango mkubwa sana hadi hapa nilipofika pia kwa sasa siwezi kutaja fedha ambayo nimeitumia hapa kwa sababu ni hela nyingi sana hadi sasa na kama unavyoona nyumba bado haijaisha kwa hiyo nikimaliza kila kitu nitasema ni shilingi ngapi nimetumia” Amesema Baraka The Price.
Hata hivyo msanii huyo aliongeza kwa kusema hivi karibuni anatarajia kufunga ndoa na penzi wake Naj baada tu ya kumaliza mjengo wake huo