Odama: Hakuna wa Kuniondolea Heshima Yangu
Staa wa Bongo Movies, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amesema kuwa tangu alipoingia katika usanii kitu kikubwa alichokuwa akikilinda ni heshima yake na si kitu kingine hivyo anayejaribu kuishusha afanye kazi ya ziada.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Odama alisema kuwa tangu ameanza kuwa msanii alijitahidi sana kuilinda heshima yake ndiyo maana watu wengi wanapenda kumjua baba wa mtoto wake lakini imekuwa vigumu.
“Watu wengi wanapenda kuishusha heshima yangu lakini nawaambia wajipange sana kwa sababu mimi ni mwanamke ninayejitambua hivyo kuishusha ni kazi ngumu sana mpaka hapa nilipofika,” alisema. Odama.
Chanzo: GPL