Ommy Alichomoa Kufundishwa Gari na Demu
Msanii Ommy Dimpoz ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake ‘Cheche’ amefunguka na kusema aligoma kabisa kujifunza au kufundishwa gari na demu wake mpaka siku alipokuja kununua gari yake ya kwanza ndipo alijifunza kupitia gari yake.
Ommy Dimpoz amesema hayo kupitia kipindi cha ‘Bongo Flava Top 20’ kinachorushwa na East Africa Radio na kudai kuwa demu wake alikuwa akimcheka sana kuona hajui gari na alikuwa akimpa sana gari yake ili ajifunze lakini yeye aligoma mpaka siku ambayo alinunua gari yake na kujifunza kupitia gari yake.
Mbali na hilo Ommy Dimpoz amefunguka kuwa mtu pekee aliyemsukuma kununua gari kwa mara ya kwanza alikuwa ni dereva bajaji ambaye alikuwa akimtumia sana kwenye safari za hapa na pale.
“Huwezi kuamini mimi nilikuwa sipendi sana kununua gari sababu nilikuwa naona maisha yangu yanakwenda maana zangu zilikuwa bajaji, sasa siku moja yule dereva bajaji aliniambia unajua wewe umekuja msanii mkubwa sana mambo ya kutumia bajaji uache sasa. Nikaona huyu mtu ambaye nampa ridhiki ananiambia maneno haya tena nikaona isiwe kesi kesho yake nikaingia mtaani na kutafuta gari, nakumbuka nilipata Rav 4 baada ya hapo ndiyo nikajifunza gari kupitia gari yangu mwenyewe” alisema Ommy Dimpoz
Aidha Ommy Dimpoz amewatoa wasiwasi mashabiki wake na kusema ‘video’ ya wimbo wake mpya ‘Cheche’ ipo tayari muda mrefu na kama mambo yatakwenda sawa basi ataachia wimbo huo wiki ijayo.
“Unajua video nilifanya kitambo toka mwezi wa Ramadhan lakini nilitaka kupima uzito wa ‘Audio’ nione je kweli watu wanapenda ‘Video’ kuliko ‘Audio’ so nilichigundua sasa ukiweka nguvu kubwa katika kufanya ‘Audio’ nzuri basi kazi itafanya vizuri tu kama ambavyo kazi yangu inafanya vyema saizi kwa sababu niliwekeza nguvu kwenye ‘Audio’ na ikitoka Video ndiyo kwanza itakuwa ngoma kama ni mpya” alisisitiza Ommy Dimpoz
EATV.TV