Gig Money: Nimekua Sitafanya Ujinga
VIDEO Queen anayezipendezesha nyimbo za wasanii Bongo, Gift Stanford, ‘Gig Money’, amesema kwa sasa amekuwa mtu mzima, hivyo hawezi kuishi maisha kama ya zamani ya kufanya matukio.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Gig Money alisema sasa ana umri mkubwa, hivyo hawezi kwenda na matukio kama aliyoyafanya zamani, kwani ule ulikuwa ni utoto.
“Sasa nimekua, najua nini maana ya maisha, hivyo siwezi kuyafanya mambo ya kitoto niliyokuwa nafanya zamani kwa sababu nahitaji muda mwingi wa kutengeneza maisha,” alisema Gig Money.
Alisema kuwa anatambua thamani ya kazi anayoifanya ya kuzipendezesha nyimbo za wasanii wenzake, hivyo atahakikisha anakaza buti ili aweze kutimiza malengo yake.
Mtanzania