-->

Ommy Dimpoz: Naijua Sababu ya Baraka Kutoka Rockstar400

MSANII wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz, anayetamba na wimbo wake mpya wa Cheche amefunguka juu ya sakata lake na Baraka Da Prince, kuwa sababu ya msanii huyo (Da Prince) kutoka katika Label ya RockStar400 ni kutokana na Ommy Dimpoz kujiunga na Label hiyo.

Ommy Dimpoz amsema si kweli kwamba yeye kuingia RockStar4000 ndiyo sababu ya Baraka Da kujua kilichomuondoa Baraka RockStar400.

“Kwanza mimi na yeye tunafanya muziki tofauti, hakuna sehemu ambayo tunaweza kusema unaweza ukatokea mkwaruzano, tunaheshimiana na mimi ni mmoja ya wasanii wenye uwezo mkubwa wa kuimba hapa Tanzania. Kwa hiyo kilichomfanya aondoke RockStar400 siwezi kukizungumzia wala kujua nini kilitokea, yeye na RockStar400 ndiyo wana majibu zaidi na sahihi,” alisema Ommy Dimpoz

Alipoulizwa iwapo RockStar400 imepata pengo baada ya Baraka kuondoka, alisema hawezi kulisemea hilo au kujua kwa sababu wakati Baraka yupo RockStar400 yeye hakuwepo kwa hiyo hajui chochote kuhusu Baraka Da Prince kuondoka RockStar400.

NA : SAMSON JEREMIAH/GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364