-->

P Funk Amuonya Master J Kuhusu Harmorapa

Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini P Funk Majani amemuonya mkongwe mwenzake katika game, Master J kutomsema vibaya kwa kumsapoti msanii Harmorapa kwa madai kuwa msanii huyo hana kipaji.

P Funkl akiwa na harmorapa ndani ya studio za FNL

P Funk pia amemkumbusha Master J jambo na kumwambia kuwa hata alipoanza kumtengeneza Juma Nature majungu na maneno yalikuwa mengi lakini alitusua na kuwa msanii mkubwa nchini.

Akiongea na eNewz ya EATV, Majani amesema kuwa yeye kama Meneja wa Harmorapa ndiye anajua ni silaha za aina gani amezitengeneza na tayari ameshamtengeneza msanii huyo kwa ajili ya mashambulizi ya kufanya vyema katika soko la muziki hivyo mtu wa nje kama kina Master J wasimuungilie.

“Unajua nilipoanza kumtoa Juma Nature waliniambia siyo msanii ila ni MC cartoon na kwamba hawezi kuwa kama Solo au Prof Jay kwa hiyo nilichekwa sana Nature pia alisemwa sana lakini nachomshukuru Mungu amenipa uwezo wa kumtambua mtu mwenye kipaji na najua huyu ata’hit au la! na kwa Harmorapa nina imani atafika mbali sana kwa hiyo J yeye asizungumze anyamaze tuu”. Alisema Majani

Katika hatua nyingine Majani amemuuelezea Harmorapa kama kijana anayestahili kuwapo kwenye sanaa hata kama si mwanamuziki lakini ni mburudishaji ambaye ana kipaji cha kuwafanya watu wafurahi hivyo hatakiwi kuwa nje ya sanaa na kwa sababu yupo tayari kwenye mikono yake anaamini atafika mbali.

“Harmorapa siyo msanii direct, kuna rapa, MC na Entertainer sasa dogo ni Entertainer. Master J kama anakumbuka kuna kipindi alimleta yule Sulukuchu studio anaimba ndugu Sulukuchu, sasa yule msanii gani lakini kuna John Walker (RIP) yule alikuwa mburudishaji kwa style yake ya ulevi kwahiyo Harmorapa anaingia kwa mtu kama Walker, watu wakipenda anachofanya ndiyo burudani yenyewe” Alisisitiza Majani.

Mkongwe huyo amesema yupo tayari kurudi kwenye game na kwa sasa anamalizia kuandaa ujio wake mpya kwa kikundi kipya cha muziki kinachoitwa Bongolos ambao anaamini watafanya vizuri sana kwenye sanaa.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364