-->

Rais Magufuli Ashiriki Ibada ya Pasaka, Awataka Watanzania Wamuombee

Dar es Salaam. Rais John Magufuli leo ameshiriki ibada ya Pasaka katika kanisa la Mtakatifu Petro na kuwashukuru wakristo na waumini wa madhehebu mengine nchini kwa kuendelea kumuombea.

Rais Magufuli akiombewa na Kardinali Pengo

Pia Rais aliwaomba waumini hao waendelee na maombi hayo ili nchi iendelee kuwa na amani, umoja, mshikamano na watu wanaochapa kazi.

Taarifa iliyoletwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu leo inaeleza kuwa Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema baraka zilizoletwa na Yesu Kristo aliyefufuka ni kwa ajili ya watu wote wakristo na wasio wakristo na amemtakia heri Rais Magufuli ili matumaini ya baraka hizo ziwafikie Watanzania wote.

Kardinali Pengo amemuombea Rais ili kuwa imara katika changamoto na machungu anayokutana nayo katika uongozi.

“Yesu Kritso akuimarishe na akutie nguvu ili matumaini tunayoyadhimisha leo yawafikie Watanzania wote”

 Chanzo:Mwananchi

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364