Picha: Odama Atoa Sadaka Kwenye Kituo cha Kulelea Watoto
Staa wa Bongo Movies, Jennifer Kyaka ‘Odama’ akiwa na wasanii wenzake siku ya jana walitembelea na kutoa sadaka kwenye kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye mazigira magumu, kituo cha Kituo Cha UMRA Kilichopo Magomeni Mikumi jijini Dar.
Odama ambaye filamu yake mpya ya MKWE imeigia sokoni hiyo jana, amewataka mashabiki wake waende madukani wakajipatie nakara halisi ya filamu hiyo kwani ni moja kati ya kazi zake bora zaidi inayosambazwa na kampuni ya steps entertainment.