-->

Q Chief Amwagia Sifa Hizi Mpenzi Wake

Msanii wa muziki Q Chief ameshindwa kuzuia hisia zake mtandaoni na kuamua kumwagia misifa mpenzi wake.

Q Chief akiwa na mpenzi wake

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Sungura, amedai mwanamke hiyo ni mwanamke wa pekee kutokana na uvumilivu wake.

“Soon tunatimiza miaka miwili katika uhusiano wetu umekuwa mvumilivu mwenye hekima ni wanawake wachache sana dunia hii wenye moyo wa chuma ulionao tumepita rough roads tumevuka vikwazo vingi tumepitia kila aina ya changamoto but most important tumepigana vita zote na kushinda sisi ni wababe wa vita love you honey, soon utatoka juani na utajikuta kivulini naamini maana Mungu wetu yu mwema nakizuri zaidi anatupenda sana,” aliandika Q Chief Instagram.

Muimbaji huyo ambaye ameweza kupambana na kuachana na matumizi ya Madawa ya kelevya, mapema mwaka 2016 alionekana akivalisha pete msichana huyo.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364