Q Chief Bado Anajuta Kuingia Kwenye Matumizi ya Madawa ya Kulevya
Ikiwa ni mwaka mmoja toka msanii wa muziki, Q Chief akiri kutumia Madawa ya kulevya na kuamua kuacha mwenyewe, muimbaji huyo bado anaumia akikumbuka jinsi Madawa ya kulevya yalivyomwaribia maisha yake.
Muimbaji huyo ambaye mpaka sasa bado ana mashabiki wengi katika muziki wake, aliacha matumizi ya Madawa ya kulevya baada ya bintie kumuelezea adha anayopata shuleni.
“Nilijiuliza kwa nini namtesa mwanangu kwa kitu kisicho na faida, nikala kiapo kuachana na ‘unga’ na ninashukuru kwa sasa nimezaliwa upya, japo kila nikikumbuka namna nilivyotaka kupoteza nakosa amani,” Q Chief aliliambia gazeti la Mwanaspoti.
Kwa sasa muimbaji huyo ambaye yupo chini QS Mhonda Entertainment anajipanga kuachia wimbo wake mpya ambao video yake ameshoot Afrika Kusini.
Bongo5