-->

Z Anto Awatolea Nje WCB

Msanii Z Anto ambaye aliwahi kutamba na ngoma kibao kali kama ‘Binti kiziwi, Mpenzi jini, Kisiwa Cha Malavidavi amefunguka na kusema kuwa mpaka sasa kuna label zaidi ya nne ambazo zinamuhitaji na kuhitaji kufanya naye kazi.

z-anto

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo Z Anto amesema alipata ofa kujiunga na WCB Wasafi lakini yeye mwenyewe anadai anatamani kufanya kazi nje ya WCB Wasafi hivyo hawezi kujiunga nao.

“Unajua mimi tatizo langu huwezi kufanya kazi kwa kubahatisha, mpaka saizi kuna ‘label’ nyingi zaidi ya tano zinanihitaji kufanya kazi, hivyo sipendi kukurupuka lazima nitulie nione nawezaje kujiunga na moja kati ya hizo. Maana nikibugi kuchagua ‘label’ ambayo inaweza kunisimamisha kufikia pale napotaka mimi nitakuwa nimejimaliza mwenyewe. Nilikuwa na maongezi na Babu Tale, nikapewa ofa kurekodi na kujinga WCB, lakini mimi natamani kufanya kazi nje ya Wasafi, nipo tayari kufanya kazi na Tip Top Connection” alisema Z Anto

Msanii huyo alitoa sababu kubwa yeye kutamani kufanya kazi nje ya Wasafi akidai tayari chini ya ‘label’ hiyo kuna mafahari hivyo hadhani kama mafahari wawili wanaweza kupatana au kwendana

“Sisi ni washairi ujue na siku zote mafahari wawili hatuwezi kufanya kazi sehemu moja, nachoweza kuwaambia ni kwamba ukimya wangu una mambo mengi mazuri na saizi kuna label moja kubwa ambayo mimi natamani kwenda kufanya nao kazi na mambo yanakwenda sawa nitakaribia kuanza nao kazi muda si mrefu’ alisema Z Anto

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364