-->

Queen Darleen Afungukia Mahusiano Yake na Alikiba

Msanii wa bongo fleva Queen Darleen amefunguka na kusema kuwa hajawahi kutoka kimapenzi na msanii Alikiba kama ambavyo watu wanazungumza na kusema ameshaambiwa anatoka kimapenzi na watu kibao akiwepo hata Diamond Platnumz ambaye ni ndugu yake.

Akiongea kwenye kipindi cha eNewz cha EATV, Queen Darleen amesema mara nyingi watu wakiona anakuwa karibu na mtu fulani huwa wanahisi kuwa ni mtu wake na hiyo ni kutokana na ukweli kwamba watu hawamjui mtu wake.

“Alikiba siyo bwana wangu na wala hajawahi kuwa bwana wangu, ila Alikiba alikuwa mshikaji wangu na zaidi ya mshikaji wangu, yaani ni ndugu kabisaa, hivyo watu waliweza kuona natoka naye kwa kuwa nilikuwa karibu naye, nazunguka naye mara kwa mara karibu sehemu zote, hivyo watu wakawa wanajua hivyo na hiyo ni kutokana na ukweli kwamba watu walikuwa hawamjui bwana wangu.” alisema Queen Darleen 

Msanii huyo alizidi kufafanua na kusema kama kweli angekuwa anatoka kimapenzi na Alikiba kipindi hicho basi hata mtoto wake angekuwa ni mtoto wa Alikiba lakini si mtoto wake kwa kuwa hawakuwa wapenzi.

“Kipindi kile nazurula sana na Alikiba mimi nilikuwa tayari mjamzito, na nisha jifungua na mtoto kwa mantiki hiyo kama Alikiba angekuwa bwana wangu basi yule mtoto angekuwa wa Alikiba, lakini mimi nilikuwa na mwanaume wangu kipindi hicho ambaye ni Hamisi Dakota hivyo watu wanaotujua sisi walikuwa wanajua jinsi gani tunavyoishi, Mimi nilishaambiwa hata Dully Skyes bwana wangu wakati yule ni kaka yangu, ikaenda wakati Nassibu anaanza kutoka nilikuwa naye karibu katika kumsaidia kazi zake watu wakasema kuwa bwana wangu” aliongeza Queen Darleen

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364