-->

Quickrocka: Kajala Hajawahi Kuwa Mpenzi Wangu

Rapa Quickrocka ambaye jana ameachia ngoma yake mpya ‘Down’ akiwa amemshirikisha msanii Mimi Mars amefunguka na kusema yeye alikuwa hatoki kimapenzi na Kajala na kusema hizo stori zilikuwa ni uongo.

Rapa Quickrocka akiwa na Kajala

uickrocka alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Friday Night Live na kusema hizo habari zilikuwa ni uongo hivyo hakuwa anatoka kimapenzi na msanii huyo wa filamu ambaye walionyesha kuwa karibu sana kipindi cha nyuma.

“Stori kuwa nilikuwa natoka na Kajala ilikuwa ya uongo, usitake nitafutia matatizo” alisema Quickrocka

Miezi kadhaa iliyopita mtaani kulikuwa na tetesi kuwa Quickrocka na Kajala Masanja ni watu ambao wanatoka kimapenzi, kutokana na ukaribu ambao walikuwa nao wasanii hao wawili huku wakionekana sehemu nyingi wakiwa pamoja, lakini tetesi hizo zimezimwa na rasmi na Quickrocka baada ya kukataa kuwa alikuwa hatoki kimapenzi na Kajala

eatv.tv

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364