Waziri Mwakyembe Akutana na Uongozi wa Simba, Wakubaliana Haya
Waziri wa Habari,Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Simba nchini.
Waziri Mwakyembe ameonana na uongozi huo ofisi kwake mjini Dodoma, Ukiongozwa na Rais wa klabu hiyo, Evans Maveva ambapo uongozi huo umetii wito wa Mheshimiwa Mwakyembe, ili kujadili mambo mbalimbali yanayohusu mpira wa miguu, zikiwemo fursa na changamoto katika uendeshaji wa timu.
Pamoja na hayo, Waziri Mwakyembe amepokea maoni ya uongozi wa Simba na kushauri kuendelea kutoa ushirikiano kwa wadau wa mpira wa miguu nchini.
Na Emmy mwaipopo
Bongo