Rais Magufuli Amteua Salma Kikwete Kuwa Mbunge
Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Mke wa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, Mama Salma kuwa mbunge wa kuteuliwa wa Bunge la Jamhuri wa Muungano Tanzania.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu usiku huu, imesema Mama Salma ataapishwa kwa mujibu na utaratibu wa Sheria zitakazotangazwa na Bunge.
Uteuzi wa Mama Salma unamfanya Rais Magufuli awe amejaza nafasi zake 8 za utuezi wa wabunge kati ya 10 kwa mujibu wa sheria.