-->

Shilole Akanusha Kutaka Kuvunja Ndoa ya Nuh Mziwanda

Msanii wa muziki na filamu Shilole amekanusha kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Nuh Mziwanda ambaye kwa sasa ameoa mwanamke mwingine aitwae Nawal.

Kupitia mitandao ya kijamii zilizagaa taarifa kwamba wawili hao wamerudia na wako karibu zaidi.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Shilole alidai kwa sasa yeye na Nuh ni washikaji na kuna baadhi ya show wanaandaa pamoja ndio maana kuna wakati wanaonekana wako pamoja.

“Mimi na Nuh sasa hivi ni washikaji, hatuwezi kugombana kama zamani, mimi na Nuh tumesaidiana vitu vingi sana kwa hiyo bado kunaushikaji fulani. Pia sisi ni wasanii, mkituona pamoja mjue kuna kazi zinaendelea, mnajua Nuh ana mke kwahiyo hayo mambo sio ya kweli, kwanza navunjaje ndoa yao?,” alisema Shilole.

Katika hatua nyingine muingaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwajili ya kazi mpya.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364