-->

Ray Atuhumiwa Uchawi, Afunguka

Staa wa filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameingia kwenye kashfa nzito baada ya kudaiwa kutumia ndumba kwenye sanaa ili kuwa juu ya wenzake, Risasi Mchanganyiko limetonywa.

ray562-1

Chanzo kutoka Bongo Muvi kilieleza madai kwamba msanii huyo mwenye jina kubwa, amekuwa ‘akiwachezea’ wenzake ili wasifanye vizuri kwenye soko la sanaa na sasa hivi ndiye anayeongoza kwa mauzo katika Kampuni ya Steps Entertainments baada ya Steven Kanumba kufariki dunia akifuatiwa kwa karibu sana na Stephen Jacob ‘JB’.
Inadaiwa kuwa moja ya viashiria vya ‘ulozi’ huo ni tukio la hivi karibuni lililotokea huko Kigamboni, ambapo tangazo lililowekwa ili kutangaza ujio wa filamu mpya ya JB, kupasuka muda mfupi tu baada ya kuwekwa.
“JB alienda kuweka bango la filamu yake ya Chungu cha Tatu maeneo ya Kigamboni lakini muda mfupi tu likapasuka katikati, lakini alipokuja kuweka Ray la kwake la Tajiri Mfupi lipo mpaka leo, hali imetutisha sana sisi wasanii,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364