Ray C bado ana ‘chumba’ Chake – Lord Eyes
Rapa Lord Eyes ambaye ni mmoja wa wasanii wa kundi la Weusi amefunguka na kusema msanii Ray C bado ana chumba chake kwenye muziki na kusema yeye bado anamuombea kwani kwa matatizo aliyonayo kwani yale ni kama maradhi hivyo hayaponi kwa siku moja.
Lord Eyes ambaye kwa sasa amepumzishwa kwenye kundi hilo, alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWZ kinachorushwa na EATV na kusema kuwa mpaka sasa yeye hawasiliani wala kuongea na Ray C na kusema ila anamuombea Mungu apone na arudi kwenye muziki kama zamani kwani nafasi yake kwenye muziki bado ipo.
“Leo hii kwenye muziki hatumuoni mtu kama Ray C, mpaka sasa hakuna mtu kama Ray C hivyo chumba chake kwenye muziki bado kipo kinamsubiri arudi tu. Sijakutana naye wala hatuongei ila namuombea Mungu kwani tatizo lile ni kama maradhi mengine hivyo haliwezi kuisha kwa mara moja linachukua muda, anahitaji maombezi na mimi namuombea kama navyojiombea mimi nifanye kazi zikamilike tukutane kwenye show huko” alisema Lord Eyes
eatv.tv