-->

Ray C Mpya Afunguka Yote Hapa

MSANII ambaye miaka kadhaa iliyopita alipotea kwenye anga la muziki baada ya kujitumbukiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, hivi karibuni alifanya mahojiano na MWANASPOTI baada ya kurudi kwenye ‘game’ la muziki na kusema haya yafuatayo:

BADO WAMO

Ray C ambaye kutokana na na kukatika, alipewa jina la ‘Kiuno Bila Mfupa’ anasema, pamoja na kupoteza muda kwenye muziki, nafasi yake bado ipo kwa upande wa wanawake kwani waimbaji wa kike wapo wachache na kila mtu ana uimbaji wa staili yake tofauti na waimbaji wa kiume.

“Najua nimepoteza muda mwingi sana katika inshu ya dawa za kulevya na kupotea katika muziki ila kwa sasa nimerudi na nafasi yangu upande wa waimbaji wa kike najua iko wazi, kwa sababu tuko wachache na kila mtu anaimba staili yake,” anasema Ray C.

HATAKI BIFU KABISA

“Sijarudi katika muziki ili niwe na mabifu na wasanii wenzangu japo ninajua ukifanya muziki mzuri na ukakubalika katika jamii, wapo baadhi ya wasanii wenzio hawawezi kukufurahia na wapo watakaokufurahia kurudi, ila kwa hilo mimi nimejipanga na sitataka kuwa na bifu na mtu kwani nubapenda amani

“Na hili suala la mabifu ni kwa hapa tu nchi yetu, lakini wenzetu huko nje ya nchi mabifu yao ni ya kuelewana na wanapiga pesa sana, yaani bifu za kibihashara na baada ya hapo utakuta watu wanapiga stori freshi tu.”

Ray C anasema kuwa, wasanii wa sasa hawana upendo na ndio maana utakuta mabifu ya kila wakati yanaibuka na hadi sasa hajajua kama wasanii wa bongo fleva Diamond na Ali Kiba hawaongei ila anahisi bifu lao litakuwa la kibihashara maana kama sio hivyo, inabidi wajiangalie mwisho wa siku wao ni kitu kimoja sababu wanafanya kazi moja.

VITU KIBAO KAMISI

Ray c amesema, kitu ambacho alikuwa anakimisi ni kile cha kukutana na wanamuziki kubadilishana mawazo ya kimuziki na upendo na ushirikiano katika wasanii tofauti ya wanamuziki wa sasa wamekuwa tofauti muziki kwao umekuwa wa kibihashara na huwezi kuta wanakusanyika kwa pamoja kila wakati.

“Yaani ilikuwa ukienda sehemu unaweza kukutana na wanamuziki zaidi ya kumi na tano na tulikuwa tuna umoja wa kukutana kila wakati kwa kubadilishana mawazo ya kimuziki yani kitu ambacho nilikuwa na kimisi mno ila wasanii wa sasa kitu hichon hakuna wamekuwa hawana upendo kwakuwa muziki wao kama nilivyosema wameufanya ni bihashara kila mtu yuko bize kutafuta mawazo ya kutengeneza kitu kizuri hivyo upendo hawana wala ile ya kukutana hawana hiyo,” alisema.

MSIKIE MWENYEWE

“Najua ninavyoendelea vizuri, ninawaponya au nimewaponya mashabiki wangu kwani ninakiri niliteleza nikaanguka, na najua mashabiki zangu walikuwa wanaumia sana na nilikuwa natokwa na machozi na kukosa raha hasa pale katika mitandao ya kijamii watu wanavyoposti vitu na mashabiki zangu wananitag au kushare, kiukweli nilikuwa nn’aumia sana

“Ila niwaambie tu kwa sasa ni kipindi cha furaha, ninamshukuru Mungu na kuwa na Imani, kwani imani ndiyo iliyonisaidia kunipa mafanikio ya uponaji, nimepitia mitihani mingi hadi kufika hapa, kiukweli, jambo la kumshukuru mungu narudia,” alisema

USHIRIKINA KWA WASANII

Ray C anasema, haamini ushirikina katika muziki, japo watu wanasema upo.

Yeye anachojua ushirikina wa kurogana ni wanamuziki au msanii anajiroga wenyewe, baada ya kutofanya bidii ya kuingia studio na kuumiza vichwa watoe kitu kizuri.

“Sidhani kama kuna ushirikina kwa wanamuziki au wasanii zaidi ya sisi wenyewe kujiroga wenyewe, yaani hapa inabidi wanamuziki tujitahidi kuingia studio tuumize vichwa kutoa kitu kizuri na sio kulalamika kurogana tu wakati kazi hazionekani,” anasema Ray C.

WATU WAMEMKAUSHIA

“Maendeleo yangu ya hali yangu ndiyo yamenifanya watu kwa sasa hawanizungumzii maisha yangu yaani saa hizi habari zangu zilizoko ni muziki na wimbo wangu mpya baada ya kupona ‘Unanimaliza,” anasema.

USHAURI WA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

Mwanamuziki huyo ametoa ushauri kwa Serikali, waweze kusaidia kuelimisha elimu mashuleni kuhusu madhara ya matumizi ya dawa za kulevya, maana wengi wanaotumia dawa hizo hawajui madhara yake na asilimia kubwa ya vijana wadogo hasa wanafunzi wanatumia muda mwingi wakati wa mapumziko kuvuta bangi na wengine dawa za kulevya bila kujua athari zake.

“Mie naiomba tu Serikali ijitahidi kutoa elimu mashuleni kuhusu athari za kutumia dawa za kulevya, kwani wengi wanaoathirika kwa sasa ni vijana tena wadogo na wengine ni wanafunzi na hao wanafunzi hutumia muda wa mapumziko kutumia dawa hizo hivyo kupewa elimu ni muhimu kwani hawajui athari zake wanajiingiza kama mimi nilivyojiingizaga bila kujua,” anasema.

AMFAGILIA LADY JAYDEE

Hata hivyo Ray C alimfagilia msanii wa kike, Lady Jay dee kwa upendo aliokuwa anautumia kipindi alipatwa na matatizo kwa kumjulia hali kila kukicha.

“Jaydee ana mapenzi ya kweli kwa msanii mwenzake. Hataki kuona anaanguka…ninampenda sana kwa moyo wake wa upendo.”

Na kuhusu kufanya nae kazi amesema japo alishawahi kufanya nae kazi hapo nyuma haikuvuma ila ana mpango wa kufanya naye kazi tena na anajua itakuwa nzuri na kukubaliwa na mashabiki na katika albamu ya Jay dee anayoipenda ni ile ya Machozi.

AZUNGUMZIA KUTOBOA VIPINI

Ray C anasema, alianza kutoboa kitovu, ulimi na chini ya mdomo tangu mwaka 2005 na alitumia muda wa dakika chache tofauti na alivyofikiria na katika hizo sehemu alizotoboa, sehemu ya kwenye kitovu ndio aliwahi kubadilisha mara kwa mara.

“Huu ni urembo tu kwangu na nilianza kutoboa hizi sehemu nakuvaa vipini tangu 2005 na katika hizo sehemu ambayo nilikuwa nabadilisha kila wakati ni kitovuni, nilikuwa ninaweka Gold au Silver,” anasema.

ANACHOPENDA NJE NA KUIMBA

Anasema, mbali na kuimba anapenda utangazaji kwani amelelewa katika mazingira ya utangazaji kabla hajaingia kuimba na alishawahi kufanya utangazaji miaka mitano Clouds FM, akaachana nayo, baada ya watu kumwambia ana sauti nzuri hasa akiimba.

RAY C NI NANI?

“Ni mtu mkali na akitaka lake hadi litimie na ni mtu wa kawaida sana na anapenda kujichanganya na watu,” anasema.

By RHOBI CHACHA, Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364