Riyama Kuja na Bonge la ‘Surprise’
MSANII wa filamu Tanzania, Riyama Ally, amesema atahakikisha anawafanyia ‘surprise’ ya kufunga mwaka mashabiki zake kwa kuachia filamu mbili matata.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Riyama, alisema amejipanga kikamilifu kabla ya mwezi huu kumalizika kuwapa zawadi hizo mashabiki zake ambazo anaamini zitakuwa za kitofauti na walivyozoea.
“Nimeamua kuwafanyia ‘surprise’ mashabiki zangu kwani bila wao mimi si kitu, hivyo zitakuwa zawadi za kipekee na tofauti ambazo sikuwahi kufanya tangu nimeanza filamu,” alisema Riyama.
Riyama aliwataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kuhakikisha wanafuatilia siku rasmi ya ‘surprise’ hiyo.
Mtanzania