-->

Riyama Kuja na ‘Matala’!

Kila unapokuta na filamu ambayo amecheza mwigizaji mahiri katika tasnia ya filamu Bongo Riyama Ali lazima ukutane na kichambo, lakini mwenye anasema kuwa amebadilika na amerudi kama zamani Riyama wa ujumbe na huzuni.

riyama3411

Riyama Ali

“Kuna wakati msanii unaigiza kulingana na uhusika wengi walinizoea kucheza sinema za kuhuzunisha lakini hapa kati nilibadilika lakini kuna filamu ya Matala wengi watalia jinsi nilivyocheza,”Riyama.

Riyama amedai kuwa katika sinema ya Matala ameigiza na kubeba ujumbe mzito sana na kubadilika kutoka kwenye kuchamba na kuwa mtu wa kuonewa na upole wa hali ya juu tofauti na muonekano wa kazi za sasa. Filamu ya Matala Riyama ameigiza kwa uigizaji wa kiwango cha hali ya juu sana na kuwaahidi wapenzi wa filamu wajiandae kuipokea baada ya kuingia sokoni.

Filamu ya Matala inasambazwa na kampuni ya Steps entertainment iewashirikisha wasanii wakali katika tasnia ya filamu Swahilihood kama vile Ahmed Ulotu ‘Mzee Chilo’, Hisany Muya ‘Tino’, Riyama Ali na wasanii wengine wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo.

FC

NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

KAMA WEWE NI MFANYA BIASHARA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364