-->

Riyama, Mumewe Wadaiwa Kutengana!

Kama kawaida, tunakuletea ubuyu wa motomoto kuwa mkali wa sinema za Kibongo, Riyama Ally na mumewe ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Haji Mwalimu Mzee ‘Leo Mysterio’, wanadaiwa kutibuana na kufikia hatua ya kutengana kimakazi.

RIYAMA934

Kisa cha yote hayo inasemekana kwamba, jamaa huyo hampendi mtoto wa Riyama aliyezaa na mwanaume mwingine, ishu ambayo mwanamama huyo amekuwa akiivumilia kwa muda mrefu lakini sasa inadaiwa kusababisha mvurugano kati yao.

SOSI AMWAGA UBUYU
Kwa mujibu wa sosi wa karibu wa wanandoa hao, hivi karibuni Riyama na Mysterio walitokea kutoelewana ndipo jamaa huyo akaondoka alikokuwa akiishi na mwanamama huyo, Mabibo, Dar na kurudi nyumbani kwao, Mbagala, jambo linalomfanya Riyama kuhaha kwani ndoa yao bado ni changa.

“Unajua Riyama anahofia watu kujua sakata la ndoa yake kwani litamchafua kwa sababu ni mtu anayependa kujistiri na kuficha mambo yake,” alinyetisha sosi huyo.

Chanzo hicho kiliendelea kufunguka kuwa, kibaya zaidi, Riyama anaogopa kuingizwa kwenye skendo ya orodha ya mastaa ambao hawatulii kwenye ndoa.

“Kiukweli inamuuma Riyama kwani ndoa yao haina hata miezi saba na hata ukimfuatilia mitandaoni hampostiposti tena Mysterio kama ilivyokuwa mwanzoni ambapo alikuwa akijitupia naye kila kukicha huku akisindikiza na baby…baby hadi kero,” kilimwaga ubuyu chanzo hicho.

RIYAMA AFIKISHIWA UBUYU
Baada ya kutonywa na chanzo hicho, Wikienda lilimsaka Riyama na kumfikishia ubuyu ambapo alifunguka anachokijua juu ya sakata hilo.

RIYAMA AFUNGUKA
“Watu wananiombea niachike. Kila siku manenomaneno…eti kisa tu simposti mtandaoni. Wakumbuke kuwa mashabiki wangu wananikubali kwa sababu ya kazi yangu siyo kupostiana na bwana kila kukicha au kumposti mtoto. Kazi ndiyo inatakiwa kupewa kipaumbele.

MWANAUME KURUDI KWAO
Wikienda: Riyama umesema kuwa humposti kwa sababu mashabiki wanataka kazi, sawa, hilo limekaa poa lakini vipi kuhusu mwanaume wako kurudi kwao Mbagala?
Riyama: Huko Mbagala amekwenda kwa sababu ya kazi yake ya muziki. Unajua studio anayorekodia ndiyo iko huko, sasa watu wakimuona wanasema tumetengana lakini ukweli kabisa hakuna kitu kama hicho.

Wikienda: Vipi kuhusu suala la mumeo kutompenda mtoto wako?
Riyama: Mh…Mimi ninachojua mume wangu anampenda mtoto kwani ndiyo roho yake.
Wikienda: Unafikiri kwa nini watu wanawapakazia jambo kama hilo wakati unasema si kweli ilihali watu wanajua wewe si mtu wa skendo?

Riyama: Nimeshasema na huo ndiyo ukweli. Unajua watu wanapenda kuyazua, ukiuliza kwa nini? Eti sijamposti mume wangu, ukurasa wangu wa Insta si kwa ajili ya mume na mtoto tu. Ni kwa ajili ya kazi zangu kwa mashabiki wangu kwani wanachotaka kuona wao ni kazi na siyo matangazo ya ndoa yangu.

Mwisho nashangaa kwa nini wananifuatafuata kwani hata kwenye ndoa yangu sikuwaalika, sasa sijui wanataka nini kwangu?
Jitihada za kumpata mwanaume huyo hazikuzaa matunda baada ya simu yake kutokuwa hewani.

NDOA YA RIYAMA INA MUDA MFUPI
Riyama (33) na Mysterio (26) walifunga ndoa Juni, mwaka huu kuelekea Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani huku Riyama akidaiwa kumzidi jamaa huyo umri hivyo kwa sasa ina miezi minne tu.

Jambo la kujiuliza ni kwa nini wanazushiwa kuwa ndoa yao imevunjika? Kama wanazushiwa, kwa nini mwanaume arudi kwao na Riyama aseme anakwenda studio?
Je, msanii akienda studio huwa harudi kwa mkewe hadi amalize kazi? Ubuyu upo mzigoni hivyo bado unaendelea kulifuatilia sakata hilo.

NENO LA MHARIRI
Ndoa nyingi za mastaa zimekuwa hazidumu lakini Riyama ni mfano wa kuigwa hivyo anapaswa kujua kuwa ndoa si jambo la mchezomchezo hivyo kama aliamua kuolewa, anatakiwa kuilinda ndoa yake ili kuwaumbua wanaoamini kuwa ndoa za mastaa hazidumu.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364