-->

Roma Aikana CHADEMA

Msanii Roma Mkatoliki ambaye anaimba muziki wa Hip hop kwenye game ya bongo, amekikana chama cha CHADEMA na kusema kuwa hajawahi kuwa mwanachama wa chama hicho kama ambavyo wengi wanaamini, na hajawahi kuwa mwanachama wa chama chochote.

Roma ambaye hivi karibuni alikutwa na sakata la kutekwa na kuibua sintofahamu nyingi, amesema kwamba hajawahi kuwa mwanasiana na hajawahi kuwa na kadi ya chama chochote.

“Mtu akisema nipo kwenye siasa za upinzani siyo jambo sahihi na siyo jambo ambalo nalifurahia kwa sababu mimi sina kadi ya chama chochote, mimi siyo mwanachama wa chama chochote, na mtu akisema nusu ya watanzania wanajua uko CHADEMA sijui ana uthibitisho gani kwa sababu sina kadi ya chama, na mimi nasimama kati kati”, alisema Roma Mkatoliki.

Roma hivi karibuni ameachia wimbo wake mpya wa ‘Zimbabwe’ ambao umeibua hisia kwa wengii, kwa kuelezea tukio zima la utekwaji wake ulivyokuwa. Wimbo ambao mpaka sasa umeweza kutazamwa na watu zaidi ya milioni moja na kitu ndani ya wiki moja.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364