Shilole: Skendo Kwangu Sasa Basi
MSANII wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, amesema sasa ameamua kutulia kuepukana na skendo, kwa kuwa tayari yupo kwenye hatua za mwisho kuingia kwenye maisha ya ndoa.
Kauli ya Shilole kudai anatarajia kuolewa hivi karibuni ilizua gumzo, huku baadhi ya watu wakidai si kweli, lakini mwenyewe amekiri kwa kusema mashabiki wake watarajie kumuona akivalishwa shela kabla ya mwaka huu kwisha.
Shilole ameliambia DIMBA Jumatano kwamba, sasa ameamua kutulia na hatasikika katika skendo yoyote, kwa kuwa anajiheshimu na ameamua kufanya maamuzi hayo kwa moyo mmoja.
“Ndoa yangu si propaganda, mimi ni mchumba wa mtu na niwaambie tu kitu kimoja, nimeamua kutulia na mume wangu mtarajiwa na msitegemee tena kusikia skendo yoyote kutoka kwangu, mara leo kwa Khamis kesho kwa Juma, hapana,” alisisitiza Shilole.
Dimba